Wednesday, April 25, 2018

SAUDI ARABIA KUMPATIA ZAWADI MO SALAH


Mohamed Salah sasa ameuwasha moto katika ulimwengu wa soka, Jana ametoka kuifungia Liverpool mabao mawili kwenye nusu fainali ya kwanza dhidi ya klabu ya Roma kutoka nchini Italia katika ushindi wa 5-2 na kufikisha magoli 43 msimu huu.


Kiwango cha jana alichokionyesha ni mwendelezo wa ambayo tumekuwa tukiyaona akiyafanya katika ligi kuu ya England EPL mpaka kuweza kubeba tuzo ya PFA ya mchezaji bora wa kiume.

Chakula aina ya Hummus Falafel hutolewa bure katika mgahawa wa Bakchich mjini Liverpool kila Mo Salah anapofunga goli, na huko nchini Misri watumiaji wa mtandao wa Vodafone  huzawadiwa dakika 11 za bure mchezajinhuyo anapocheka na nyavu.

Kama ulistaajabu hayo basi utaendelea kustaajabu kwani Mo Sala naye anaendelea kuonyesha ubora wake.
Kiwango chake cha hali ya juu kimelifanya taifa lake la Misri na mataifa ya Kiarabu kujivunia na Salah
Katika hatua ya kumpongeza kwa kiwango chake, makamu raisi wa mji takatifu wa Mecca huko Saudi Arabia,  Fahad Al Rawky amesema Mo Salah atapatiwa Kipande cha Ardhi Mjini humo kama Zawadi kwa ushindi wa tuzo ya PFA.

Lakini fahad amesema kama haitowezekana kumpa Ardhi basi utajengwa Msikiti na utapewa jina lake.